1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne ajiuzulu

9 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne amewasilisha kwa Rais Emmanuel Macron uamuzi wa kujiuzulu kwa serikali yake.

https://p.dw.com/p/4b0K5
Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne akiwa mjini Paris
Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne akizungumza Bungeni mjini Paris: 20.03.2023Picha: Lewis Joly/AP Photo/picture alliance

Jina la mrithi wa Elisabeth Borne, mwenye umri wa miaka 62 na ambaye amekuwa mwanamke wa pili katika historia ya Ufaransa kushikilia wadhifa huo, linatarajiwa kutangazwa rasmi hii leo.

 Lakini kulingana na vyanzo vya kuaminika, Macron anatarajiwa kumteua katika nafasi hiyo Waziri wa Elimu Gabriel Attal.

Macron yuko katika jitihada za kuitakasa serikali yake ambayo imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kufuatia kupitishwa Bungeni kwa mswada wa uhamiaji ambao ulifanyiwa mabadiliko makubwa na yenye utata yaliyoshinikizwa na wapinzani wa mrengo wa kulia.