1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Palestina ajiuzulu

26 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu na serikali yake katika hatua ambayo huenda ikafunguwa njia ya mageuzi yanayoungwa mkono na Marekani.

https://p.dw.com/p/4csv5
Waziri Mkuu wa Palsetina, Mohammed Shtayyeh.
Waziri Mkuu wa Palsetina, Mohammed Shtayyeh.Picha: THOMAS KIENZLE/AFP

Uamuzi huo wa kujiuzulu kwa Shtayyeh lazima ukubaliwe Rais Mahmoud Abbas kabla ya kutekelezwa kwake.

Hatua hiyo inaashiria nia ya uongozi huo wa Palestina unaoungwa mkono na nchi za Magharibi kukubali mabadiliko ambayo yanaweza kuleta mageuzi yanayoonekana kuwa muhimu katika kuifufua serikali ya Mamlaka ya Palestina.

Soma zaidi: Watu 25 wauawa katika mapigano ya Israel na wapiganaji wa Gaza

Marekani inataka serikali ya Palestina iliyofanyiwa mageuzi kuutawala Ukanda wa Gaza mara baada ya kumalizika kwa 
vita vya Israel kwenye Ukanda huo, lakini bado kuna vikwazo vingi katika kutimiza matakwa hayo.