1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Waziri Mkuu Pakistan aamuuru kukamatwa waliohusika na ghasia

13 Mei 2023

Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif amewaamuru polisi kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika katika vitendo vya ghasia baada ya waziri mkuu wa zamani, Imran Khan kukamatwa mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/4RJ9l
Pakistanischer Ex-Premier Khan vorübergehend freigelassen
Picha: W.K. Yousafzai/AP/dpa/picture alliance

Wafuasi wa Khan waliokuwa wanapinga kukamatwa kwake siku ya Jumanne kwa madai ya ufisadi, na kusababisha ghasia za nchi nzima. 

Wafuasi hao walivamia majengo ya jeshi na kuchoma moto jengo la kituo cha televisheni ya taifa, wakaharibu mabasi, walipora kwenye nyumba ya afisa wa juu wa jeshi na kuziharibu mali nyingine, hatua iliyosababisha kukamatwa kwa watu 2,000 na jeshi kusambazwa kwenye miji kadhaa. 

Takribani watu wanane waliuawa katika ghasia hizo. 

Khan aliyeachiliwa kwa dhamana jana, baadae leo anatarajiwa kuwahutubia wafuasi wake kwa njia ya mtandao. 

Aidha, huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, YouTube na Twitter haipatikani tena kuanzia leo, baada ya huduma hiyo kurejea tena jana usiku.