1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Waziri mkuu wa Kosovo awasilisha mpango wa suluhu ya amani

13 Juni 2023

Waziri mkuu wa Kosovo Albin Kurti leo amewasilisha mpango wake wa suluhu ya kumaliza mvutano katika eneo tete la Kaskazini mwa Kosovo linalokaliwa na idadi kubwa ya jamii ya Waserbia.

https://p.dw.com/p/4SWmf
Kosovo Pristina | EU-Sonderbeauftragter Miroslav Lajcak und US-Sonderbeauftragter Gabriel Escobar
Picha: Erkin Keci/AA/picture alliance

Sehemu ya mpango huo ni kufanyika uchaguzi mpya wa serikali za mitaa pamoja na kuondolewa kwa askari wa kikosi maalum.

Hatua ya waziri mkuu Kurti imekuja baada ya kushinikizwa na washirika wake muhimu wa nchi za magharibi waliounga mkono uhuru wa jimbo hilo.

Wakati huohuo Polisi wa Kosovo wamesema wamemkamata mtu mmoja kutoka jamii ya Waserbia ambaye serikali ya Pristina imemtambua kama, Milun Milenkovic aliyeshiriki kuandaa mashambulio dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Jumuiya ya NATO, waliopelekwa kaskazini mwa Kosovo mwezi uliopita baada ya kuzuka machafuko.

Eneo hilo la kaskazini lilitumbukia kwenye vurugu baada ya mabaraza yote ya miji kuwekwa mameya wenye asili ya Kialbania.