1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Kosovo yalaani taarifa za kukamatwa kwa maafisa wake watatu

16 Juni 2023

Kosovo imesema itaongeza ulinzi katika mpaka wake na Serbia wakati ambapo nchi hizo mbili zinalaumiana kwa kutumiana vikosi vya watu waliojihami.

https://p.dw.com/p/4Sfsy
Mvutano kati ya Serbia na Kosovo unaibua kitisho cha kuibuka kwa vita vya kati ya mwaka 1998 na 99 na kusababisha vifo vya maelfu ya raia.
Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti amelaani taarifa za kukamatwa kwa maafisa wake watatuPicha: Erkin Keci/AA/picture alliance

Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti amelaani taarifa za kukamatwa kwa maafisa wake watatu wa polisi kulikofanywa na maafisa wa Serbia. Kurti ametaja tukio hilo kama utekaji nyara na kudai kwamba lilitokea ndani ya Kosovo. Waziri Mkuu huyo amekosoa hatua ya walinda amani wa kimataifa wanaoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO waitwao KFOR, kwa kushindwa kutangaza msimamo wao kuhusiana na tukio hilo. Tukio hilo linaongeza mvutano uliopo kati ya pande hizo mbili ambao umegeuka na kusababisha machafuko katika miezi kadhaa iliyopita. Machafuko hayo yamesababisha hofu ya kuzuka tena kwa mapigano kama yaliyotokea kati ya mwaka 1998 na 99 nchini Kosovo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 10.