Kosovo: Genge la uhalifu lahusika shambulizi la Septemba
23 Oktoba 2023Waziri mkuu wa Kosovo amedai hii leo kwamba genge la wahalifu kutoka kaskazini mwa Serbia lilihusika na shambulizi la mwezi Septemba lililosababisha kifo cha polisi mmoja na mapigano makali yaliyodumu kwa siku nzima na polisi wa Kosovo, ambapo watu watatu waliuawa.
Waziri Mkuu Albin Kurti pia amedai kwamba Waziri wa Ulinzi wa Serbia Milos Vucecic ndiye anayeongoza kundi hilo linaloitwa Novi Sad Clan, na kuongeza kwamba Rais wa Serbia Aleksandar Vucic pia alikuwa na mahusiano na kundi hilo. Hata hivyo hakutoa ushahidi wa madai hayo.
soma pia:Uingereza yatuma wanajeshi wake kulinda amani Kosovo
Wizara ya ulinzi ya Serbia imekana tuhuma hizo na kumtuhumu Kurti kwa kusema uongo, huku ikiiomba jamii ya kimataifa kuzuia kile ilichoita kampeni "chafu na za uchochezi" za uongozi wa Kosovo.
Mapigano hayo yalirejesha wasiwasikati ya Kosovo na Serbia na yalikuwa mabaya kabisa kushuhudiwa tangu Kosovo ilipopata uhuru kutoka kwa Serbia 2008.