1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Waziri mkuu wa Japan aanza ziara ya ghafla Ukraine

21 Machi 2023

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameanza ziara yake ya kushtukiza nchini Ukraine leo Jumanne saa chache baada ya rais wa China Xi Jinping kuwasili katika nchi jirani Urusi kwa ziara ya siku tatu.

https://p.dw.com/p/4Oyaq
Japan Tokio | Premierminister Fumio Kishida, Ankündigung Ideen für Russland-Sanktionen
Picha: Stanislav Kogiku/AP Photo/picture alliance

Ziara hizo za kilele  zinakuja katika wakati ambapo mahasimu hao wa muda mrefu wako katika mapambano ya kuoneshana nguvu kidiplomasia. Waziri mkuu Kishida wa Japan atakutana na rais Volodymyr Zelensky mjini Kiev.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Japan,  kiongozi huyo  ataonesha mshikamano na uungaji mkono kwa Ukraine,  na kuupongeza ushujaa na subira ya waukraine waliosimama kidete kuitetea nchi yao chini ya uongozi wa rais  Zelensky.

Katika mazungumzo yake anatarajiwa pia kuipinga Urusi na uvamizi wake nchini Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW