1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Waziri Mkuu wa Italia kuitembelea Ukraine

21 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni anakwenda mjini Kyiv leo kwa mazungumzo na rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine yanayolenga kuonesha mshikamano na taifa hilo lililo vitani.

https://p.dw.com/p/4NmaP
Deutschland | Besuch italienische Premierministerin Giorgia Meloni in Berlin
Picha: Michael Sohn/AP Photo/picture alliance

Meloni anaizuru Ukraine baada ya kuitembelea Poland hapo jana ambako alitoa ahadi kwamba Italia itaendelea kuisaidia serikali mjini Kyiv ikiwa ni pamoja na msaada ziada wa kifedha, kijeshi na ule wa kiutu.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia aliyechukua hatamu za uongozi nchini Italia Oktoba iliyopita, alizungumzia mara kadhaa dhamira yake ya kuitembelea Ukraine kuonesha mshikamano na nchi hiyo kufuatia uvamizi wa Urusi.

Italia iliyo mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO tayari imeipatia Ukraine msaada wa fedha na silaha na mapema mwezi huu iliridhia kutuma mfuko wa kujilinda na makombora ulioundwa kwa pamoja kati ya nchi hiyo na Ufaransa.