1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Blinken akamilisha ziara ya Mashariki ya Kati

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati iliyokuwa na lengo la kuzuia mapigano baina ya Israel na Hamas kugeuka kuwa mzozo wa kikanda.

https://p.dw.com/p/4b9OZ
 Antony Blinken mjini Cairo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiondoka CairoPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati iliyokuwa na lengo la kuzuia mapigano baina ya Israel na Hamas kugeuka kuwa mzozo wa kikanda.

Ziara ya Blinken IsraeBlinken aiambia Israel iepuke 'madhara zaidi kwa raia' Gazal: 

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuondoka mjini Cairo Misri, Blinken alisema kuwa vita vya Gaza havipanuki na kumekuwa na hatua mathubuti kuelekea utatuzi wa mzozo huo.

Miongoni mwa hatua hizo ni makubaliano ya Israel ya kuruhusu timu ya Umoja wa Mataifa, kufanya tathmini kaskazini mwa Gaza ili kuangalia mazingira ya kuanza kuwaruhusu watu kurejea kutoka upande wa kusini.

Blinken pia amesema nchi za kanda hiyo zimekubali kushirikiana na kuratibu juhudi za pamoja kwa ajili ya Gaza, amani na utulivu wa muda mrefu katika eneo hilo.