1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Blinken afanya mazungumzo kwa siku ya pili Beijing

19 Juni 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakamilisha hii leo ziara yake nchini China na amediriki siku ya pili na ya mwisho ya mikutano muhimu na maafisa wakuu wa Beijing

https://p.dw.com/p/4SkTI
China USA l US-Außenminister Antony Blinken trifft Staatschef Xi
Picha: Leah Millis/Pool/AFP via Getty Images

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakamilisha hii leo ziara yake nchini China na amediriki siku ya pili na ya mwisho ya mikutano muhimu na maafisa wakuu wa Beijing, katika dhamira ya kupunguza mvutano inayoongezeka kati ya Marekani na China.

Mataifa hayo mawili yamedhihirisha nia ya kuendelea na mazungumzo licha ya kushindwa kuafikiana kuhusu masuala muhimu yanayopelekea kuongezeka kwa mivutano.

Soma pia: Blinken awasili China kupunguza joto la mivutano

Miongoni mwa mambo hayo ni masuala ya biashara, mzozo wa Taiwan, haki za binaadamu nchini China na Hong Kong pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Blinken alikutana na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi kwa takriban saa tatu, na atakutana na Rais Xi Jinping kabla ya kuondoka leo jioni.

AP