1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Baerbock aitaka Afrika Kusini kuamua kuhusu Ukraine

26 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock ameitolea mwito Afrika Kusini kuulewa msimamo wa Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi katika nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4T3il
London Ukraine Recovery Conference Baerbock
Picha: Henry Nicholls/PA Wire/picture alliance

Baerbock ametowa mwito huo Jumapili akizungumza na gazeti moja la mjini Johannesberg, kabla ya ziara yake nchini Afrika Kusini.

Waziri huyo wa Ujerumani anatarajiwa Jumanne kwenda Afrika Kusini ambako atakuwa na mazungumzo na waziri anayehusika na masuala ya uhusiano wa kimataifa wa nchi hiyo, Naledi Pandor mjini Pretoria.

Baerbock amesema juhudi za amani za bara la Afrika katika mgogoro wa Ukraine zilizoongozwa na Afrika Kusini zinaweza kuwa fursa ya kuonesha ushawishi wa  Afrika Kusini na kwamba sauti ya nchi hiyo ina nguvu katika jukwaa la kimataifa. Pia amesema katika ziara yake nchini humo mikataba kadhaa kuhusu ushirikiano itasainiwa kati ya nchi hizo mbili.