1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Wawili kuchuana na Putin uchaguzi wa rais mwezi Machi

5 Januari 2024

Tume ya uchaguzi nchini Urusi leo imeidhinisha wagombea wawili wa urais ambao watashindana na Rais Vladimir Putin katika uchaguzi mkuu utakaofanyika katikati ya mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/4auNy
Rais Vladimir Putin wa Urusi
Rais Vladimir Putin wa Urusi atawania muhula wa tano madarakani wakati wa uchaguzi wa mwezi Machi.Picha: Kristina Kormilitsyna/dpa/picture alliance

Tume hiyo ya uchaguzi imemuidhinisha Leonid Slutsky wa chama cha kizalendo cha LDP na Vladislav Davankov kutoka chama kinachoitwa "Watu Wapya."

Wagombea hao wawili hawaonekani kuwa tishio kwa Putin ambaye ametawala siasa za Urusi tangu alipoingia madarakani mnamo mwaka 2000.

Vyama vya wagombea hao kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikiunga mkono sheria zinazopendekezwa bungeni na chama cha Putin cha United Russia.

Hata hivyo, mwanasiasa Yekaterina Duntsov ambaye anahimiza kusitishwa kwa vita nchini Ukraine hajaidhinishwa kuwania urais.