1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawaniaji wa Kombe la Dunia Afrika sasa waangazia AFCON

17 Novemba 2021

Timu zote 10 isipokuwa moja tu ambazo zimefuzu hatua ya mwisho ya mechi za kufuzu katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa upande wa Afrika zitakuwa na kibarua kingine cha kushughulikia kabla ya kujua atakayetua Qatar.

https://p.dw.com/p/436Jq
Fußball | Africa Cup 2017 | Togo vs Elfenbeinküste
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Timu zote 10 isipokuwa moja tu ambazo zimefuzu hatua ya mwisho ya mechi za kufuzu katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa upande wa Afrika zitakuwa na kibarua kingine cha kushughulikia kabla ya kuamuliwa nani atakayepanda ndege kwenda Qatar 2022.

Algeria, Cameroon, Misri, Ghana, Mali, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia zipo kwenye mkondo sahihi wa kutua Qatar lakini zitashiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Junuari kabla ya kuangazia sasa shughuli ya kufuzu Kombe la Dunia mwezi Machi.

Ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pekee ambao wametinga duru ya mwisho ya kufuzu kucheza Qatar licha ya kushindwa kufuzu Afcon.

Timu zitapangwa katika makundi mawili ya timu tano ambapo kutakuwa na mechi za mikondo miwili, nyumbani na ugenini na washindi wataiwakilisha Afrika nchini Qatar. Mechi hizo za mikondo miwili zitachezwa kati ya Machi 24 na 29.

Hivi ndivyo itakavyokuwa kwenye makundi hayo

Pot 1

Senegal

Tunisia

Algeria

Nigeria

Morocco

Pot 2

Misri

Ghana

Cameroon

DR Congo

Mali

Reuters