1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wavamizi wachoma basi na kuwauwa abiria 30 nchini Nigeria

8 Desemba 2021

Takriban abiria 30 wameungua moto hadi kufa ndani ya basi katika jimbo la Sokoto nchini Nigeria baada ya watu waliojihami kwa silaha jana Jumanne kulichoma moto.

https://p.dw.com/p/43z9V
Nigeria Abuja | Sicherheitspersonal | Entführte Studenten
Picha: Nasu Bori/AFP/Getty Images

Polisi na wakaazi wa eneo hilo wamesema tukio hilo ni moja kati ya mengine yanayokumbusha kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi katika jimbo hilo la kaskazini magharibi, Sanusi Abubakar, basi hilo lilikuwa na abiria 24 wakati lilipochomwa moto na watu saba ndani ya basi hilo walifanikiwa kutoroka wakiwa na majeraha na kupelekwa hospitali.

Lakini wakaazi wawili ambao walifika katika eneo la tukio na kusaidia kuondoa miili waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba basi lilikuwa limejaa abiria zaidi na miili iliteketezwa moto kiasi cha kutoweza kutambuliwa.

Walihesabu sehemu za miili ya angalau watu 30, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.