1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu wakusanyika kwa ajili ya ibada mlima Arafa

Hawa Bihoga
15 Juni 2024

Waumini wa Kiislamu zaidi ya milioni 1.5 watakusanyika na kufanya ibada katika mlima Arafa wakati kukiwa na kiwango kikubwa cha joto linaloongezeka na ikiwa ni siku muhimu zaidi katika ibada hiyo ya hija ya kila mwaka.

https://p.dw.com/p/4h4ve
Makka, Saudi Arabia | Mahujaji wakiwasili Mina
Mahujaji wakiwa wanaenlekea MinaPicha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Waumuni hao kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni  watakwea mlima huo wenye futi 230, ikiwa ni takriban kilometa 20 kutoka mji Mtakatifu kwa Waislamu wa Makka ambako Mtume Muhammad anaaminika kutoa mahubiri yake ya mwisho.

Joto la jangwani majira ya kiangazi linatarajiwa kufikia nyuzi joto 43 katika kipimo cha Selsiasi, na kuwa chagizo miongoni mwa wazee katika siku hii muhimu na kudurusu Kurani.

Soma pia:Mahujaji wa Kiislamu wajiandaa kwa ibada rasmi ya Hija

Mamlaka ya Saudia imewataka mahujaji kunywa maji mengi na kujikinga na jua.

Ibada ya hija ni miongoni mwa nguzo tano katika dini ya Kiislamu na hufanywa kwa wale wenye uwezo kiuchumi na afya njema.