1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waukraine wakimbia makaazi yao kutafuta usalama kwengine

12 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa unasema Waukraine milioni 6.2 wameikimbilia nchi za nje kufuatia uvamizi wa Urusi nchini humo

https://p.dw.com/p/4Yiak
Makaazi ya kupokea wakimbizi mjini Berlin, kutoka Ukraine
Wakimbizi kutoka Ukraine waliokimbilia Ujerumani wakiwa katika makaazi ya muda BerlinPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Takriban watu milioni 5 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao nchini Ukraine, na kuelekea kwenye maeneo mengine ya nchi hiyo kufuatia miaka kadhaa ya mashambulizi ya Urusi,hayo ni kwa mujibu wa takwimu rasmi za nchi hiyo.

Makamu waziri mkuu anayehusika na masuala ya wakimbizi Iryna Vereshchuk amemesema kwamba kuna wakimbizi milioni 4.9 wa ndani waliosajiliwa huku kiasi ya  milioni 3.6 wakiwa wamekimbilia katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo tangu uvamizi wa Urusi Februari 2022. Soma pia: UNHCR: Watu milioni 110 walazimika kukimbia makazi yao

Kabla ya uvamizi huo,mapigano ya miaka kadhaa katika jimbo la Donbass,mashariki mwa Ukraine yalikuwa tayari yameshasababisha zaidi ya watu milioni 1 kuwa wakimbizi wa ndani tangu mwaka 2014.

Kwa mujibu wa takmwimu za Umoja wa Mataifa za hivi karibuni takriban Waukraine milioni 6.2  wamekimbilia nchi za nje ama kwa muda au kubakia kabisa walikokimbilia.