1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waturuki wanapiga kura leo

14 Mei 2023

Vituo vya kupigia kura leo hiii vimefunguliwa kote Uturuki kwa uchaguzi muhimu wa bunge na urais utakahamua hatma ya siku zijazo za taifa hilo lenye kuunganishwa na mabara mawili - Ulaya na Asia.

https://p.dw.com/p/4RKDa
Türkei | Wahlen 2023 | Erdogan
Picha: Umit Bektas-Pool/Getty Images

Takriban watu milioni 61 wametimiza vigezo vya kupiga kura, wakiwemo wapya karibu milioni tano watakaopiga kura kwa mara ya kwanza. Waturuki walio nje ya nchi tayari wametimiza wajibu wao huo wa msingi. Mchakato huo unatazamwa kuwa na matokeo muhimu zaidi baada ya miongo miwili ya rais wa sasa wa taifa hilo, Recep Tayyip Erdogan, ambapo waangalizi kadhaa wa kimataifa wakiwa tayari wametawanywa katika taifa hilo.Mgombea wa muungano wa upinzani na kiongozi wa chama cha CHP, Kemal Kiliçdaroglu, anachuana na Erdogan, wanayemtaja kuwa kama shujaa wa uhafidhina wa Kiislam.