1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Watu wawili wauawa katika shambulizi la angani Syria

4 Aprili 2023

Raia wawili wa Syria wameuwawa katika shambulizi la kutokea angani, shambulizi la nne la aina hiyo dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serikali chini ya kipindi cha wiki moja katika nchi hiyo inayokabiliwa na vita

https://p.dw.com/p/4PfpX
Syrien Irak l US Air Force - US Navy F-18E
Picha: Staff Sgt. Shawn Nickel/US AIR FORCE /AFP

Raia wawili wa Syria wameuwawa katika shambulizi la kutokea angani mapema leo, shambulizi la nne la aina hiyo dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serikali chini ya kipindi cha wiki moja katika nchi hiyo inayokabiliwa na vita.

Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kwamba jeshi la Israel limefanya shambulizi hilo la kutokea angani lililosababisha vifo vya raia hao wawili, likinukuu duru ya jeshi.

Shambulizi hilo limetokea upande wa milima ya Golan inayokaliwa na Israel, ikiyalenga maeneo kadhaa karibu na mji mkuu Damascus na eneo la kusini.