1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Watu wawili wauawa karibu na mpaka wa magharibi wa Urusi

30 Aprili 2023

Maafisa wa Urusi wamesema watu wawili wameuawa kwenye mpaka wa magharibi wa jimbo la Bryansk baada ya kushambuliwa kwa makombora na majeshi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Qj3Q
Russland, Bryansk | Brand in einem Öllager
Picha: Max Kirilovky/ITAR-TASS/IMAGO

Gavana wa jimbo hilo la Bryansk ametoa taarifa hiyo na kusema majeshi hayo yaliteketeza jengo la makaazi na nyumba nyingine mbili kwenye kijiji cha Urusi cha Suzemka.

Hapo jana Jumamosi moto mkubwa ulizuka katika rasi ya Crimea inayodhibitiwa na Urusi baada ya shambulizi linaloshukiwa kuwa la ndege isiyo na rubani kupiga ghala la mafuta, huku mapigano yakipamba moto katika eneo la kusini mwa Ukraine.

Soma pia: Urusi yajiandaa kukabiliana na mashambulizi ya Ukraine

Mnamo siku ya Ijumaa, wanajeshi wa Urusi walishambulia jengo la ghorofa katikati ya mji wa Uman nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu 23 akiwemo mtoto mchanga.