1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 3 hawajulikani walipo baada ya kutokea kimbunga Uswisi

23 Juni 2024

Watu watatu hawajaweza kufahamika walipo baada ya kutokea dharuba ya katika maeneo ya mabonde ya Graubünden na Valais, katika kipindi hiki ambacho pia kumekuwa na mvua za hapa na pale katika maeneo mengi ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4hOnQ
Uswisi, Graubünden | baada ya dhoruba
Dhoruba nyingi za radi na mvua kubwa katika bonde la Uswizi la Graubünden na Valais. Picha: Jean-Christophe Bott/keystone/dpa/picture alliance

Safari za treni zilianza tena katika mji wa Zermatt huko Valais karibu na eneo la  Matterhorn, ambalo ni kivutio maarufu cha watalii, baada ya kukatizwa kwa zaidi ya masaa 24.

Reli mbili na barabara inayoingia mjini ilikuwa imezuiliwa kwa muda baada ya mikondoya kingo za mito ikipasuka. Katika kijiji cha Graubünden, kilichopo mpakani na Italia huku watu watatu wanaendelea kutafutwa baada ya nyumba zao kuharibiwa na maporomoko ya ardhi ya Ijumaa.