1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watano wauawa katika mlipuko wa bomu mashariki ya Kongo

20 Juni 2024

Takribani watu watano, wameuawa katika shambulio la bomu kwenye mji wa Kanyabayonga wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4hIRj
Mzozo wa mashariki ya Kongo
Umoja wa Mataifa umesema watu milioni 1.5 wamekiyambia makazi yao mashariki ya Kongo.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Kongo katika eneo la Kivu Kaskazini Mak Hazukay amewalaumu waasi wa M23 kwa kuhusika na shambulio hilo. Hazukay amesema watu watatu wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Soma pia: AU walaani mauaji ya watu wengi nchini DR Congo

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, vifo hivyo vinaonyesha hali mbaya inayowakabili wananchi kutokana na mgogoro wa zaidi ya miaka miwili kati ya majeshi ya Kongo na wanamgambo wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu milioni 1.5 wamekiyambia makazi yao mashariki ya Kongo.