1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Temeko la ardhi laua watu 15 nchini Ecuador na Peru

19 Machi 2023

Watu 15 wamekufa na wengine 400 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter lilizozipiga jana nchi za Ecuador na Peru.

https://p.dw.com/p/4OuLG
Ecuador I Erdbeeben
Picha: Gleen Suarez/AFP/Getty Images

Watafiti wa Jiolojia wa Marekani wamesema tetemeko hilo lilipiga pwani ya Ecuador katika mkoa wa Guayas.

Idadi kubwa ya vifo kufuatia tetemeko hilo imeshuhudiwa nchini Ecuador ambapo rais wa nchi hiyo Guillermo Lasso akitoa wito wa utulivu na kuyatembelea majimbo yaliyoathiriwa zaidi ya El Oro na Azuay.

Ecuador na Peru zinapatikana katika sehemu inayojulikana kama "Gonga la Moto la Pasifiki", ambalo hukumbwa mara kwa mara na matetemeko ya ardhi kutokana na kuhifadhi takriban volkano 128.