Watu wanne wauawa kufuatia mashambulizi ya roketi huko Lviv
6 Julai 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya ndani ya Ukraine na kubaini kuwa shughuli ya uokoaji bado inaendelea.
Zaidi ya watu saba wameokolewa kutoka kwenye vifusi huku wengine 60 wakihamishwa kutokana na nyumba zao kuharibiwa.
Meya wa Lviv, Andriy Sadovyi, amesema ni shambulio baya zaidi dhidi ya miundombinu ya raia wa Lviv tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi ambapo zaidi ya nyumba 50 zimeharibiwa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram kuwa bila shaka kitendo hicho alichokiita "shambulio la magaidi wa Urusi" kitajibiwa.