1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Watu takribani 100 wamekufa kufuatia ajali ya boti Nigeria

14 Juni 2023

Takribani watu zaidi ya 100 wamekufa na wengine kadhaa kutojulikana walipo baada ya boti waliokuwemo kuzama huko katika eneo la kaskazini ya kati ya Nigeria.

https://p.dw.com/p/4SXoQ
Nigeria Boote in Lagos
Picha: Emmanuel Osodi/UIG/IMAGO

Duru zinaeleza boti ya mbao iiliyojaa watu kupita kiasi ilikuwa ikiwavusha watu kwa kutumia mto kutoka jimbo la Kwara kwenda jimbo la Niger, baada ya hafla  ya harusi.

Haikuweza kufahamika mara moja ni watu wangapi walikuwa ndani boti, lakini serikali ya jimbo la Kwara  katika taarifa ilisema watu walikuwa kutoka vijiji vitano na juhudi za uokoaji kwa haraka iwezekanavyo kwa manusura zilikuwa zikiendelea.

Kwa kuhofia magenge ya wenye kujihami kwa silaha raia wengi wa Nigeria wanatumia usafiri wa boti lakini pamoja na hilo msongamano na matengenezo duni ni chanzo cha vyombo vingi vya majini kusababisha ajali.

Matumizi ya boti na mashua kusuluhisha msongamano wa magari Lagos