1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 8 waliozama ziwa Victoria Kenya waendelea kutafutwa

22 Septemba 2021

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya mashua kwenye Ziwa Victoria, Homabay nchini Kenya imefikia watatu baada ya mwili mmoja zaidi kupatikana Jumatano.

https://p.dw.com/p/40eeF
Turning the ominous hyacinth into manure
Picha: DW

Juhudi za kuitafuta miili zaidi zinaendelea ila zoezi hilo linakabiliwa na chagamoto za hali mbaya ya hewa na magugu maji iliyochangia kusitishwa kwa juhudi hizo. Mashua hiyo ilizama Jumanne jioni.

Miili ya abiria wawili kati ya abiria 16 waliokuwa wamepanda mashua hiyo iliyokuwa inasafiri kutoka Piya Homabay mjini kuelekea Ndhuru - Mbita Kusini kilomita 12 kutoka ufuoni, ilipatikana jana.

Abiria wengine sita waliokolewa na wavuvi na kukimbizwa hospitalini.

Mkurugenzi idara ya majanga Homabay, Eliud Onyango amesema oparesheni hiyo inaongozwa na maafisa wa mamlaka inayosimamia uchukuzi majini kwa ushirikiano na asasi ya ulinzi wa fukwe za bahari na kitengo kinachosimamia fukwe za ziwani.