1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 71 wauawa baada ya shambulizi la Israel, Gaza

13 Julai 2024

Kiongozi wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Deif anaaminika kuwa miongoni mwa wahanga wa shambulizi la anga la Israel ambalo mamlaka ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza

https://p.dw.com/p/4iFuz
Watu wapatao 71 wamefariki kufuatia shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza
Watu wapatao 71 wamefariki kufuatia shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Gaza Health Ministry Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Kiongozi wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Deif anaaminika kuwa miongoni mwa wahanga wa shambulizi la anga la Israel ambalo mamlaka ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza imeripoti kuwa watu 71 wameuawa na mamia kujeruhiwa.

Gazeti la Haaretz la nchini Israel limesema vyanzo vya jeshi vinaamini kuwa kiongozi huyo wa al-Qassam Brigades aliuawa katika shambulio hilo.

Soma zaidi. Miili 60 yapatikana baada ya operesheni ya Israel

Kwa upande wake, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema kuwa shambulizi lilimlenga Deif na kiongozi mwingine wa kundi hilo katika mji wa Rafa Salama katikati ya Khan Younis. Ingawa bado hawajathibitisha iwapo viongozi hao wawili ambao wanatajwa kuwa walitengeneza mpango wa tukio la Oktoba 7 mwaka uliopita wamefariki.

Jeshi la Israel limesema lililenga eneo la Hamas na hakukuwa na watu katika eneo hilo kwa hivyo waathirika huenda pia wakawa ni wanachama wa kundi hilo ingawa ripoti za ndani ya Palestina zinadai kuwa shambulizi hilo limelenga makazi na mahema ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao.