1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yasema haijapokea taarifa kutoka kwa wapatanishi

11 Julai 2024

Kundi la Hamas limesema kuwa wapatanishi wa mzozo kati ya Israel na kundi hilo bado hawajatoa taarifa zozote kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza.

https://p.dw.com/p/4iBdR
Qatar, Doha | Viongozi wa Hamas
Viongozi wa Kundi la Hamas linalopigana na vikosi vya Israel Ukanda wa Gaza wakijadili mapendekezo ya usitishwaji mapigano.Picha: HAMAS MEDIA OFFICE/REUTERS

Katika taarifa yake iliyoitoa leo Hamas pia imeishutumu Israel kwa mkwamo uliopo, ili kupata wakati na kuzuia duru ya sasa ya mazungumzo, kama ilivyofanya katika duru zilizopita. 

Hamas imetoa matamshi hayo wakati wapatanishi wa Qatar na Misri, wakiungwa mkono na Marekani, wakiongeza juhudi wiki hii ili kukamilisha makubaliano ya kusitisha mapigano yenye lengo la kumaliza vita vya miezi tisa huko Gaza. 

Soma pia:UN yaonya kuhusu IDF kuwataka raia kuondoka Ukanda wa Gaza

Pia kwa lengo la kuwaachilia huru mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas na Wapalestina wengi waliofungwa jela nchini Israel.