JamiiUfaransa
Watu 667 wakamatwa kote Ufaransa kufuatia ghasia za umma
30 Juni 2023Matangazo
Maelfu ya waandamanaji wenye hasira wamechoma moto majengo kadhaa na kupambana na maafisa wa usalama ili kulaani kisa hicho.
Jumla ya watu 667 wamekamatwa kote nchini Ufaransa. Maafisa wa polisi wapatao 294 wamejeruhiwa kufuatia vurugu hizo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Ufarasa Gérald Darmanin amesema serikali imetawanya maafisa 40,000 wa polisi nchi nzima kujaribu kutuliza vurugu za maelfu ya watu wanaodai haki ya mvulana aliyeuwawa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu Elisabeth Borne, wameitisha mkutano wa dharura ili kujadili vurugu hizo ambazo zimeripotiwa katika miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Paris, Marseille, Lille, Lyon, Bordeaux na Grenoble na pia katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.