1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 60 wahofiwa kufa Nepal baada ya mabasi kusombwa na maji

12 Julai 2024

Maporomoko ya ardhi katika eneo la kati la Nepal yameyasomba mapema leo mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba karibu abiria 60 katika mto uliokuwa umefurika.

https://p.dw.com/p/4iDMj
Nepal l Maporomoko ya ardhi
Waokoaji wakitafuta manusura katika mto Trishuli huko NepalPicha: Rajesh Ghimire/AFP/ via Getty Images

Maporomoko ya ardhi katika eneo la kati la Nepal yameyasomba mapema leo mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba karibu abiria 60 katika mto uliokuwa umefurika. Mvua zinazoendelea kunyesha na maporomoko zaidi ya ardhi yanazidisha ugumu katika juhudi za uokoaji.Watoto 68,000 Nepal wahitaji msaada

Watu watatu walionusurika wanaripotiwa kuogelea hadi sehemu salama ila waokoaji wanasema hadi kufikia mapema leo, hawajafanikiwa hata kuona dalili za mabasi hayo ambayo huenda yamezama na kupelekwa katika eneo la chini la mto Trishuli. Maji katika mito ya Nepal kwa kawaida huwa yana kasi kutokana na kuwa ardhi hiyo ni ya milimani. Mabasi hayo yanasemekana yalikuwa katika barabara kuu inayounganisha Mji Mkuu Kathmandu na maeneo ya kusini ya Nepal ndipo yaliposombwa na maporomoko hayo ya ardhi.