1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuAfrika Kusini

Watu 6 wauwawa mauaji ya holela Afrika Kusini

12 Agosti 2023

Polisi nchini Afrika ya kusini wameanzisha msako mkubwa wa kuwatafuta wanaume wanne wanaotuhumiwa kuwauwa kwa bunduki watu sita kwa madai kwamba watu hao waliiba kitambulisho.

https://p.dw.com/p/4V6AS
Südafrika | Schüsse in einer Bar in Soweto mit mindestens 15 Toten
Picha: Ihsaan Haffejee/AFP/Getty Images

Watuhumiwa wanaotafutwa walivamia nyumba moja  kwenye kitongoji kilicho karibu na mji Durban Ijumaa usiku na kufanya mauaji hayo.

Msemaji wa polisi Robert Netshiunda amesema uchunguzi wa awali unaonesha kiongozi wa kundi lililofanya mauaji aliwataka wahanga kumpatia kitambulisho chake inachosemekana alikipoteza kwa bahati mbaya .

Ripoti zinaonesha kuwa mtuhumiwa huyo aliamini kwamba mmoja kati ya watu aliowauwa aliokota kitambulisho hicho.  Netschiunda amesema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa akitafutwa na polisi kuhusiana na mauaji mengine.

Mauaji ya watu wengi kwa wakati mmoja hutokea mara kwa mara nchini Afrika kusini, taifa ambalo ni moja ya nchi zenye kiwango kikubwa zaidi cha mauaji duniani.