1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Watu 6 wauwawa kwenye shambulio la kisu nchini China

10 Julai 2023

Watu 6 wameuwawa leo na mwengine mmoja amejeruhiwa katika shambulizi la kutumia kisu lililotokea kwenye shule moja ya awali huko kusini mwa China.

https://p.dw.com/p/4TemZ
China, Peking
Mtu akiendesha baiskeli na mtoto wake katika jimbo la GuangzhouPicha: Aly Song/REUTERS

Watu 6 wameuwawa leo na mwengine mmoja amejeruhiwa katika shambulizi la kutumia kisu lililotokea kwenye shule moja ya awali huko kusini mwa China.

Gazeti la serikali la China limenukuu duru za polisi zikisema mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa kuhusiana na shambulizi hilo katika mji wa Lianjing uliopo ndani ya jimbo la Guangzhou.

Hakuna maelezo ya ziada yaliyotolewa lakini mashuhuda kadhaa ambao hawakutambulishwa majina wamesema mtoto wa mshambuliaji aligongwa na gari la mmoja ya waliouwawa muda mfupi kabla ya shambulio hilo. Inaarifiwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni mwalimu mmoja wa shule hiyo.

Soma pia: Shambulio la risasi lachochea maandamano Hong Kong

Mashambulizi ya kutumia visu yanayozilenga shule za chekechekea yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini China na mengi huchochewa na nia ya mshambuliaji kulipa kisasi.