1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 6 wamekufa pwani ya Myanmar kufuatia kimbunga

15 Mei 2023

Takriban watu 1,000 wameokolewa upande wa magharibi mwa pwani ya Myanmar kufuatia kimbunga kikali kilichopiga eneo hilo na kuwajeruhi mamia na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano.

https://p.dw.com/p/4RMNL
BG Zyklon Mocha in Bangladesch und Myanmar
Picha: Al-emrun Garjon/AP/picture alliance

Tayari watu saba wameripotiwa kupoteza maisha yao, japo athari halisi ya kimbunga hicho bado haijajulikana katika nchi hiyo ambayo ni moja kati ya nchi zenye maendeleo duni barani Asia.

Upepo mkali umewajeruhi zaidi ya watu 700 kati ya 20,000 waliokuwa wamejihifadhi katika maeneo ya nyanda za juu katika kitongoji cha Siitwe.

Maji yalikuwa yamejaa kiasi cha kina cha mita 1.5 juu ya ardhi katika maeneo yaliyofurika japo shughuli za uokoaji zingali bado zinaendelea.