1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 32 wauwawa katika mapigano ya kikabila Sudan

20 Novemba 2023

Mashambulizi kutoka kwa makundi hasimu ya kabila la Dinka katika eneo linalozozaniwa na Sudan pamoja na Sudan Kusini, yamesababisha mauaji ya watu 32 mwishoni mwa juma.

https://p.dw.com/p/4ZEec
Sudan | Pichani ni wanawake wa kijiji cha Kassala
Sudan | wanawake wakiwa katika kijiji chao cha KassalaPicha: Eric Lafforgue/imago images/Hans Lucas

 

Bulis Koch, Waziri wa habari wa eneo la Abyei amesema siku ya Jumapili asubuhi kundi la vijana la Twic Dinka linaloungwa mkono na wanamgambo wa ndani lilivishambulia vijiji vya watu wa kabila la Ngok Dinka Kaskazini Mashariki mwa mji wa Agok.

Soma pia:Ujumbe wa UN watakiwa kumaliza shughuli zake Sudan

Msemaji wa jeshi la Sudan hakujibu ombi la Reuters kutaka maoni juu ya taarifa hii. Sudan Kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe muda mfupi baada ya Sudan kujipatia Uhuru wake mwaka 2011.

Makubaliano ya amani yaliyosainiwa miaka mitatu iliyopita inaendelea kuwepo lakini serikali ya mpiti imekuwa ikichukua hatua ndogo ya kuunganisha makundi kadhaa ya jeshi.