1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 30 wauawa Nigeria

17 Mei 2023

Takriban watu 30 wameuawa katika mashambulizi kwenye vijiji vya kaskazini mwa Nigeria katika jimbo la Plateau.

https://p.dw.com/p/4RUMl
Nigeria Jos City Plateua State
Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Mamlaka nchini Nigeria zimesema baadhi ya nyumba zilichomwa moto.

Gavana wa jimbo la Plateau ameviagiza vikosi vya usalama kufanya msako wa kuwatafuta watu waliofanya mashambulio hayo.

Maeneo ya kaskazini magharibi na katikati ya Nigeria kwa muda mrefu yamekabiliwa na mapigano kati ya wakulima na wafugaji wanaogombea maji na ardhi.

Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mgogoro huo.

Msemaji wa polisi, Alfred Alabo, amesema amri ya kutotoka nje kwa saa 24 imewekwa katika eneo la Mangu ili kuepuka kuenea kwa mgogoro huo.