1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Watu 30 hawajulikani walipo baada ya mashua kuzama

13 Machi 2023

Watu 30 hawajulikani walipo baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Mediterania. Boti hiyo ilikyouwa ikisafiri kutoka Libya ilizama kutokana na hali mbaya ya hewa.

https://p.dw.com/p/4Oahy
Italien Mittelmeer Flüchtlingsboot vor Kalabrien
Picha: Handout Guardia Costiera/AFP

Mashua ya wahamiaji kutoka Libya iliyokuwa ikielekea nchini Italia imepata ajali siku ya Jumapili katika bahari ya Mediterania.

Hadi sasa watu 30 haijulikani walipo. Walinzi wa Pwani ya Italia wamefahamisha kuwa watu wengine 17 wamefanikiwa kuokolewa na kuwa shughuli za uokoaji zinaendelea.

Kwa mujibu wa shirika la hisani la Mediterranea Saving Humans, mashua hiyo ilipinduka takriban maili 110 kaskazini-magharibi mwa Benghazi.

Idadi ya wahamiaji wanaoingia Italia kutoka Afrika Kaskazini na Uturuki imeongezeka maradufu mwaka huu, lakini mamia ya wahamiaji wengine wamekufa wakati wakijaribu kuvuka na kuingia barani Ulaya kupitia njia hatari ya bahari ya Mediterania.