1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 27 wafa baada ya mashua kuzama katika pwani ya Tunisia

9 Aprili 2023

Watu 27 wamekufa baada ya mashua mbili kuzama katika pwani ya Tunisia. Watu wengine 53 waliokolewa katika kadhia hiyo.

https://p.dw.com/p/4PquI
MSF Rettungsschiff Geo Barents
Picha: Salvatore Cavalli/AP/picture alliance

Watu 27 wamekufa baada ya mashua mbili kuzama katika pwani ya Tunisia. Watu wengine 53 waliokolewa katika kadhia hiyo. Maafisa wa Tunisia wamesema watu hao kutoka katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara walikuwa wanasafiri kwenda Ulaya. Matukio hayo ya hatari ni miongoni mwa mengine kadhaa katika wiki chache zilizopita. Maafisa wa Tunisia wameripoti ongezeko la mara tano katika shughuli za uokoaji ikilinganishwa na mwamnzoni mwa mwaka jana. Pwani za Tunisia, ipo umbali wa kilomita 150 tu kutoka kisiwa cha Lampedusa nchini Italia, na hutumiwa zaidi na raia kutoka nchi za Afrika Magharibi, Sudan na wengineo wanaofanya safari hizo hatarishi kujaribu kufika barani Ulaya kutafuta usalama na maisha bora.