1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMyanmar

Watu 26 wameuwawa katika mapigano Myanmar

15 Juni 2023

Mapigano makali kati ya jeshi la Myanmar na makundi ya wapiganaji yamesababisha vifo vya takriban raia 26, wakiwemo watoto sita, katika eneo la mashariki mwa mji mkuu wa taifa hilo Naypyidaw.

https://p.dw.com/p/4Sadn
Myanmar | Maandamano
Waandamanaji wakitumia vizimia moto kukabiliana na polisi 2021Picha: STR/AFP/Getty Images

Mapigano makali kati ya jeshi la Myanmar na makundi ya wapiganaji yamesababisha vifo vya  takriban raia 26, wakiwemo watoto sita, katika eneo la mashariki mwa mji mkuu wa taifa hilo Naypyidaw.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa wakazi, makundi ya haki za binaadamu na watoa tiba. Mapigano hayo yametokea katika kitongoji cha Pekon katika Jimbo la Shan, ambalo limekuwa na makabaliano ya mapambano yaliyoibuka baada ya Februari 2021 wakati jeshi lilipochukua mamlaka kutoka kwa serikali ya kiraia ya Aung San Suu Kyi.

Soma hapa: Myanmar yakumbuka miaka miwili ya mapinduzi ya kijeshi

Makundi ya kikabila yamekuwa yakipigana na serikali kuu kwa zaidi ya nusu karne, kutafuta uhuru zaidi katika maeneo makubwa wanayoishi..