1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 25 wauwawa nje ya mji wa Donetsk unaodhibitiwa na Urusi

21 Januari 2024

Watu 25 wameuwawa kufuatia kombora lililorushwa katika soko moja nje ya mji wa Donestsk katika eneo linalodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4bVss
Donetsk
Watu 25 wauwawa nje kidogo ya mji wa Donetsk unaodhibitiwa na UrusiPicha: Dmitry Yagodkin/TASS/dpa/picture alliance

Denis Pushilin, mkuu wa utawala wa Urusi mjini Donestsk amesema watu wengine 20 wakiwemo watoto wawili wanasemakana kujeruhiwa katika shambulio hilo lililofanyika katika eneo la Tekstilshchik. 

Makombora ya Urusi yawajeruhi watu 11 mjini Kharkiv

Pushilin amedai mashambulizi hayo yamefanywa na jeshi la Ukraine. Hata hivyo Kiev haijatoa tamko juu ya madai hayo.