1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Watu 25 wauawa katika shambulio la makombora mjini Donetsk

22 Januari 2024

Takriban watu 25 wameuawa katika shambulio la makombora kwenye soko lililoko katika mji wa Donetsk unaokaliwa na Urusi, mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4bWVK
Soko la Merkury lililoshambuliwa kwa makombora
Soko la Merkury lililoshambuliwa kwa makomboraPicha: Dmitry Yagodkin/TASS/dpa/picture alliance

Kiongozi anayeungwa mkono na Urusi katika mji wa Donetsk Denis Pushilin, amesema kuwa watu wengine 20 wakiwemo watoto wadogo wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Ameongeza kuwa, askari wa Ukraine ndio waliofanya shambulio katika soko hilo lenye shughuli nyingi. Jeshi la Ukraine hata hivyo halijatoa kauli yoyote juu ya shambulio hilo.

Baadhi ya vyombo vya habari vya Ukraine vimeonyesha picha na vidio za soko lililoharibiwa vibaya.

Meya wa mji wa Donetsk Alexey Kulemzin amelaani shambulio hilo na kuliita la "kinyama" lililofanywa na askari wa Ukraine.