1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi: Watu 24 washtakiwa kwa kujihusisha na ushoga

9 Machi 2023

Duru za mahakama nchini Burundi zimefahamisha kuwa watu 24 wameshtakiwa kwa kushiriki vitendo vya mapenzi ya jinsia moja wakati serikali ya taifa hilo la kihafidhina, ikiendesha msako dhidi ya watu wa jamii ya LGBTQ

https://p.dw.com/p/4ORMs
Symbolbild Afrika Homosexualität
Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Polisi iliwakamata wanaume 17 na wanawake saba mnamo Februari 23 kwenye warsha katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega, iliokuwa imeandaliwa na shirika la hisani la MUCO Burundi, linaloangazia VVU na ugonjwa wa Ukimwi.

Soma pia: Utetezi wa Tutu wa mashoga haukuwashawishi Waafrika wengi

Hapo jana jioni, Armel Niyongere, mkuu wa kundi la haki za binadamu ACAT Burundi, alisema baada ya kuhojiwa kwa takriban siku 10, watu hao walishtakiwa na mwendesha mashtaka wa umma kwa kukuza mapenzi ya jinsia moja na kujishughulisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vilivyoorodheshwa kama uhalifu unaobeba hukumu ya kifungo gerezani chini ya sheria ya Burundi.