1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaLibya

Watu 2,000 wahofiwa kufariki Libya kufuatia Kimbunga Daniel

12 Septemba 2023

Maafisa nchini Libya wamesema usiku wa kuamkia Jumanne kuwa karibu watu 2,000 wanahofiwa kuwa wamefariki kutokana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha.

https://p.dw.com/p/4WDdA
Libyen Nach Überschwemmungen in der Stadt Derna
Picha: AA/picture alliance

Mafuriko hayo yameshuhudiwa baada ya kimbunga Daniel kuipiga kanda ya Bahari ya Mediterrania. Taarifa hiyo ya vifo vya watu 2,000 imetolewa na Waziri Mkuu wa serikali ya Mashariki mwa Libya Ossama Hamad alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha al-Masar. Kiongozi huyo ameongeza pia kuwa kati ya  watu 5,000 na 6,000 hadi sasa haijulikani waliko.

Mkurugenzi mmoja wa shirika la kimataifa la misaada ameiambia DW kwamba Libya inashuhudia maafa makubwa. Uharibifu mkubwa zaidi umeshuhudiwa katika jiji la Derna kwenye jimbo la Jabal al-Akhdar na katika viunga vya Al-Marj.

Vikosi vya uokoji vimepelekwa kwenye mji huo, ulioko takriban kilometa 900 mashariki mwa mji mkuu, Tripoli.