1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Watu 16 wamekufa katika ajali ya mgodi wa makaa nchini China

25 Septemba 2023

Watu 16 wamekufa jana Jumapili katika ajali ya mgodi wa makaa ya mawe katika mji wa Panzhou, mkoa wa Guizhou kusini magharibi mwa China

https://p.dw.com/p/4WlXS
Waokoaji wa China wanambeba mchimba migodi aliyeokolewa kutoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Qianqiu ulioporomoka katika mji wa Yima, mkoa wa kati wa China wa Henan, 5 Novemba 2011.
Waokoaji wa China wanambeba mchimba migodi aliyeokolewa kutoka kwenye Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Qianqiu Picha: picture-alliance/dpa

Shirika la habari la serikali ya China Xinhua, limefahamisha kuwa shughuli za uokoaji katika mgodi huo zinaendelea, na kwamba kikosi maalum kimetumwa katika mkoa wa Guizhou ili kuratibu juhudi za uokozi. Serikali imetangaza pia hatua za kuboresha usalama katika sekta hiyo.

Panzhou ina uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha makaa ya mawe

Jiji la Panzhou lina uwezo wa kuzalisha kwa mwaka takriban tani milioni 52.5 za makaa ya mawe ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya kupikia, ikiwa ni karibu asilimia 5 ya uwezo jumla wa uzalishaji wa makaa ya mawe nchini China. Februari mwaka huu watu 53 walikufa katika ajali kama hiyo huko Mongolia.