1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 12 wafariki katika msongamano huko Madagascar

Sylvia Mwehozi
26 Agosti 2023

Watu 12 wamekufa katika msongamano mkubwa wa watu katika uwanja wa michezo nchini Madagascar wakati mashabiki walipokusanyika kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Visiwa vya Bahari ya Hindi.

https://p.dw.com/p/4VbIY
Madagaskar Antananarivo | Mahamasina Stadion
Picha: Frederic Dugit/maxppp/picture alliance

Watu 12 wamekufa katika msongamano mkubwa wa watu katika uwanja wa michezo nchini Madagascar wakati mashabiki walipokusanyika kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Visiwa vya Bahari ya Hindi.

Waziri Mkuu wa Madagascar Christian Ntsay amesema watu wengine takribani 80 wamejeruhiwa, 11 kati yao wako katika hali mbaya. Rais wa Madagascar Andry Rajoelina alikuwepo katika sherehe hizo katika uwanja wa Mahamasina katika mji mkuu wa Antananarivo.

Uwanja huo, ambao umejengwa kuchukua watu wapatao 41,000, umekuwa chanzo cha watu kukanyagana na kusababisha madhara. Mtu mmoja alifariki na wengine 37 walijeruhiwa katika ghasia za kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika kati ya Madagascar na Senegal mwaka wa 2018. Mwaka 2019, takriban watu 15 walikufa uwanjani kutokana na kukanyagana wakati wa tamasha la muziki.