1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

29 Desemba 2023

Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi la Urusi nchini Ukraine. Hayo yameelezwa hii leo na maafisa wa Ukraine huku idadi ya vifo ikihofiwa kuongezeka.

https://p.dw.com/p/4ahBe
Ukraine | Jengo lililoshambuliwa na makombora ya Urusi
Jengo lililoshambuliwa na makombora ya UrusiPicha: Ukrainian Emergency Service/AP/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi imefyetua makombora 110 leo Ijumaa.

Gavana wa mkoa wa katikati mwa Ukraine wa Dnipropetrovsk, Sergiy Lysak, amesema watu wanne wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa eneo hilo. Viongozi wengine wameripoti vifo vya watu kadhaa katika mikoa ya Odesa, Kharkiv, Lviv na hata mji mkuu Kyiv.

Soma pia: Urusi yaivurumishia mvua ya makombora Ukraine

Ukraine imekuwa ikionya kwa wiki kadhaa kwamba Urusi inaweza kuanzisha mashambulizi makubwa ya anga na kuilenga miundombinu yake ya nishati.

Katika msimu wa baridi wa mwaka jana, mamilioni ya watu nchini Ukraine walikosa umeme kutokana na mashambulizi ya Urusi.