Watigray wanaolinda amani UN wahofia kurejea Ethiopia
25 Februari 2022Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa wameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba Umoja wa Mataifa umeshindwa kuunga mkono kikamilifu mamia ya wanajeshi wenzao wa kabila la Tigray wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wakihofia kurejea nyumbani Ethiopia na kukabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vizuizi huku kukiwa na mzozo katika jimbo la Tigray nchini humo.
Akaunti zao zinaonesha wasiwasi uliopo miongoni mwa watu wa Tigrayan baada ya maelfu ya wanajeshi na raia kuzuiliwa kote Ethiopia baada ya vita vya nchi hiyo kuzuka Novemba 2020 kati ya vikosi vya Ethiopia na wapiganaji kutoka mkoa wa Tigray.
Idadi isiyojulikana imetolewa wiki za hivi karibuni baada ya mapigano mengi kupungua ambapo imepelekea wiki hii Ethiopia kuondoa hali ya hatari.
Soma pia→Ethiopia: Wapiganaji wa Tigray walaumiwa kwa ubakaji
Nini kimetokea hadi hayo yanajiri?
Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Tigray waliiambia AP kwamba wao na mamia ya wafanyakazi wenzao wamemaliza muda wao wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huko Abyei, eneo linalopiganiwa na Sudan na Sudan Kusini, na sasa wanatarajiwa kurejea Ethiopia.
Walidai kuwa kambi yao ya kulinda amani iko chini ya udhibiti wa Ethiopia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa hawaruhusiwi kuifikia.
Sgt. Angesom Gebru, ambaye alitoroka kutoka kambi hiyo pamoja na wengine kadhaa, alisema walinda amani Tigrayan wa waliosalia wanaweza tu kuondoka salama mara watakapopelekwa kwenye uwanja wa ndege wa ndani, kwa safari za ndege kurejea Ethiopia, iliyoanza wiki hii.
Lakini kwa vile watu wa Tigray wanakataa kupanda ndege hizo, alisema, kuna hofu kwamba wale ambao bado wako kwenye ulinzi wa amani kambi yao inaweza kukabiliana na kisasi.
Makumi ya wanajeshi wa kulinda amani wa jamii ya Tigrinya walifanya maandamano kupinga vita nchini Ethiopia wiki hii. Picha iliyopigwa na kusambazwa na Angesom inawaonyesha wanaume na wanawake, wakiwa na alama ya blue nembo ya Umoja wa Mataifa ikiwaonesha wamesimama na ishara iliyoandikwa kwa mkono inayosomeka ``Komesha mauaji ya kimbari huko Tigray.''
Soma pia→Asilimia 40 ya watu wa Tigray wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula
Maeneo yanayo zuiliwa na Ethiopia
Eneo la Tigray lenye takriban watu milioni 6 limezuiliwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya Ethiopia tangu Juni mwaka jana huku mamlaka ikidai kuwa misaada ya kibinadamu au vifaa vingine vinaweza kutumika kusaidia vikosi vya Tigray.
''Mafuta, pesa taslimu na vifaa vinavyopatikana kwa washirika wa maswala ya kibinadamu huko Tigray vimekaribia kuisha,'' shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu liliripoti wiki iliyopita.
Walinda amani wawili waliiambia AP kwamba mamlaka ya Ethiopia katika kambi hiyo iliwaambia watu wa jamii ya Tigrinya kwamba hawatadhurika iwapo watarejea nyumbani.
Katika taarifa iliyotolewa kwa shirika la habari la Associate Press,msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa alisema ''baadhi ya walinda amani wamechagua kutorejea na wanatafuta ulinzi wa kimataifa na wanalindwa na Umoja wa Mataifa katika eneo salama."
Msemaji huyo alisema "Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana katika ngazi zote ili kuruhusu askari wa kulinda amani kufanya uamuzi huru wa kurejea makwao au kutafuta hifadhi kutokana na hofu ya kurejea nyumbani".
Soma pia :Ethiopia yapitisha sheria ya kuanza tume ya majadiliano ya kitaifa
Tayari mamia warejeshwa
Mnamo Februari 2021, idadi kubwa ya wanajeshi wa kabila la Tigrinya walioko kwenye ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini walikataa kupanda ndege kurejea nyumbani kurejea katika makazi yao. Na mwezi Aprili, msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq alisema idadi kadhaa ya Waethiopia wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur nchini Sudan walitafuta ``ulinzi wa kimataifa'' huku mamia ya wanajeshi wakirejeshwa makwao.