1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watekaji nyara wa Mmarekani nchini Niger wataka fidia

29 Oktoba 2020

Watu wenye silaha waliomteka nyara raia wa Marekani Philip Walton kusini mwa Niger, wamedai fidia ili wamuachilie huru. Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/3kbuG
Niger Armee | bewaffnete Truppe
Picha: AFP/S. Ag Anara

Philip Walton, anaelezewa kuwa ni mtoto wa mmishonari anayeishi Niger, alitekwa nyara Jumatatu usiku na wanaume sita wakiwa wamebeba silaha nzito nje kidogo ya Massalata, kijiji kilicho karibu na mpaka wa Nigeria. Watu waliomteka tayari wameshampigia baba yake kudai fidia hiyo.

Vikosi zaidi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo, na juhudi za pamoja kati ya vikosi vya Marekani na Nigeria zinaendelea kumtafuta raia huyo wa Marekani aliyetekwa nyara.

Niger ni taifa lilioko katikati mwa eneo la Sahel, ambalo limegubikwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi yenye itikadi kali za kidini ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine kuyahama makazi yao.