1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu wataka vikosi vya Mali na Wagner vichunguzwe

1 Februari 2023

Wataalamu huru wa haki za binaadamu wanataka vikosi vya serikali ya Mali na wapiganaji wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner Group wachunguzwe kwa makosa yanayohusiana na uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/4Mxvv
Russland Sankt Petersburg 2022 | PMC Wagner Centre
Picha: Igor Russak/REUTERS

Wataalamu huru wa haki za binaadamu wametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu uwezekano wa unyanyasaji, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu unaofanywa na vikosi vya serikali ya Mali na wapiganaji wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner Group. 

Wataalamu hao wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa wamesema wamepokea taarifa kuhusu mauaji ya kutisha, makaburi ya watu wengi, ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa katika kipindi cha miaka miwili kwenye mji wa Mopti na maeneo mengine ya Mali. 

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wataka kuchunguza mauwaji ya Mali

Wamesema wana wasiwasi kwamba shughuli za kijeshi zinakabidhiwa kwa kikosi mamluki cha Wagner, jambo linalochochea vurugu. 

Kwa mujibu wa wataalamu hao, kuna hali ya ugaidi na kulipiza kisasi dhidi ya watu wanaojaribu kuzungumza na tayari wamewasilisha taarifa hizo kwa serikali ya mjini Bamako.