1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wataalamu wa amani, usalama Maziwa Makuu wakutana Bujumbura

4 Machi 2024

Wataalamu wanaohusika na masuala ya amani na usalama pamoja na kukabiliana na migogoro wanakutana kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kutathmini njia za kumaliza mizozo kwenye nchi wanachama.

https://p.dw.com/p/4d9vI
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amekuwa mwenyeji wa mkutano wa watalaamu wa amani na usalama wa kanda ya maziwa makuu.Picha: Tchandrou Nitanga/AFP/Getty Images

Wataalamu wanaohusika na masuala ya amani na usalama pamoja na kukabiliana na migogoro wanakutana kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kutathmini njia za kumaliza mizozo iliyopo kati ya nchi wanachama wa Kanda ya Maziwa Makuu na machafuko ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma pia: UN yawahimiza viongozi wa Maziwa Makuu kumaliza mizozo

Huang Xia, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye kanda ya Maziwa Makuu amesema hali si ya kuridhisha katika nchi za eneo hilo kutokana na migogoro isiyokwisha na pia machafuko huko mashariki mwa Kongo, licha ya nchi za kanda hiyo kutia saini makubaliano ya amani na usalama.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Albert Shingiro, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi 13 za Kanda ya Maziwa Makuu na Afrika Kusini zilizotia saini na Kongo amesema licha ya mkataba huo kutiwa saini zaidi ya miaka kumi sasa, kuna changamoto zinazo kwamisha utekelezaji wake.