1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasifu wa kiongozi wa chama cha FDP Guido Westerwelle

Aboubakary Jumaa Liongo14 Septemba 2009

Miongoni mwa vyama vinavyowania kuingia madarakani katika uchaguzi wa sept 27 ni chama cha FDP kinachoongozwa na Guido Westerwelle na ambacho hadi sasa ni nguzo ya tatu katika siasa za Ujerumani

https://p.dw.com/p/JeVa
Kiongozi wa chama cha FDP Guido WesterwellePicha: AP

Mara ya mwisho kwa chama cha FDP kushiriki katika serikali ilikuwa mwaka 1998.Lakini kwa sasa kiongozi na mwenyekiti wa chama hicho Guido cha Kiliberali Westerwelle anajiwinda kukirejesha tena chama chake hicho serikalini.

HISTORIA YAKE

Westerwelle ana umri wa miaka  47 tu lakini tayari amekwishajiwekea rekodi ya kuongoza chama hicho kwa muda mrefu .Kiongozi pekee wa chama hicho cha FDP  aliyewahi kukaa madarakani kwa muda mrefu ni  Hans-Dietrich Genscher aliyekuwa madarakani kuanzia mwaka 1974 hadi 1985.

Westerwelle amekuwa madarakani kuanzia mwaka  2001.Katika mkutano mkuu uliyopita wa chama hicho uliyofanyika mjini Hannover, Westerwelle alichaguliwa tena kukiungoza kwa wingi mkubwa wa karibu asilimia 96 ya kura.Ni kiongozi wa  awabunge wa FDP katika  bunge la Ujerumani Budestag tangu mwaka 2006.

HANA MPINZANI KATIKA CHAMA

Wakati vyama vingine vidogo  chama cha Kijani -Grüne-na kile cha mrengo wa shoto -Linke-, wamekuwa  na kinyanganyiro cha uongozi wa juu na kulazimika kuwa na viongozi wawili washirika, Guido Westewelle anakiongoza FDP peke yake. 

Parteitatg Bündnis 90/Die Grünen: Spitzenkandidaten Renate Künast und Jürgen Trittin
Viongozi wa muungano wa vyama vya kijani na Linke Renate Kuenast, kushoto na Juergen Trittin kuliaPicha: AP

Chama cha kijani kinaongoza na Renate Künast na Jürgen Trittin kwa pamoja na Linke  Gregor Gysi na Oskar Lafontaine .

Chini ya Uongozi wa Westewelle FDP kimepiga hatua kubwa. Wakati aliposhika uongozi  chama hicho kilishindwa kuongoza katika  mikoa mingi. Hayo yalionekana katika kipindi cha miaka 30 ya kua mshirika katika serikali kuu hadi 1998.

Lakini katika kipindi cha Westewelle sasa  ni mshirika katika serikali nyingi za mikoa ,  kikipata ushindi mmoja baada ya mwengine  huku mkubwa zaidi ukiwa katika mkoa wa Nordrhein Westfalen wenye wakaazi milioni 17.

MAFANIKIO

katika miaka minne iliopita, FDP kimegeuka kuwa chama  chenye nguvu cha upinzani katika bunge la shirikisho mjini Berlin. Kuna uwezekano kikawa na nafasi ya kurudi madarakani kwa kushirikiana na chama cha CDU.

Pindi hilo litatokea na kuundwa serikali ya muungano wa CDU na FDP Westerwelle anaweza kuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje na makamu wa Kansela, nyadhifa ambazo kijadi  zimekua zikishikiliwa na Waliberali walipokua  serikalini.

1969 hadi 1998 nyadhifa hizo mbili zilishikiliwa na Walter Scheel, Hans Dietrich-Genscher na Klaus Kinkel. Genscher ambaye ni kivutio cha Westewelle alishika nyadhifa hizo mbili kwa pamoja kwa muda wa miaka 18.

Westerwelle anahitaji miaka mingine mitatu kufikia rekodi ya Genscher  ya kukiongoza chama cha FDP. Genscher alikua kinara kwa miaka 11.

Mwandishi: Fürstenau,Marcel/ZR/Aboubakary Liongo

Mhariri:M.Abdul-Rahman