1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mjadala juu ya John Bolton kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa wa Marekani utaendelea mwezi ujao

27 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9l

Baada ya mjadala mkali hapo jana jioni kati ya wabunge wa Marekani,bunge limeshindwa kufikia uamuzi juu ya chaguo la rais Gorge Bush John Bolton kuwa balozi katika Umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Kura 42 za chama cha upinzani cha Demokrats dhidi ya kura 56 zimeweza kutoa nafasi ya kuendelea kwa mjadala huo.

Chama hicho cha upinzani kilihitaji kura za wabunge 41 kuzuia kuendelea kwa kura ya kumuidhinisha bwana Bolton kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani.